K
Habari zenu wasomaji wangu!
Kama kawaida leo tunakutana tena ulingoni…. Katika kuwekana
sawa hapa na pale kwenye masuala ya urembo masuala ya usafi na kadhalika! Mradi
kwa gharama ndogo tu unabaki msaaafi kabisa na mwenye furaha tele! Team kubana matumizi hahahaha!
Leo nataka kugusia suala la makwapa kuwa meusi.
Inakera sana!...
hasaaa linapokuja suala la kuvaa nguo ya kukata mikono. Yaani unakosa
kujiamini. Tena basi uwe kwenye
kadamnasi ambapo unatakiwa kupunga mikono hivi…ni zaidi ya shughuli!... unashindwa hata kujimwayamwaya mwenzangu aiiii kisa tukwapa tweusi!
Kuwa na kwapa jeusi sio ugonjwa, sio dhambi lakini mwenzangu
linapunguza maksi kiasi fulani…. Halafu kwanini uwe na lami makwapani wakati
njia tele za kuondoa na kuzuia zimejaaaa!!
Kwanza tuangalie sababu za makwapa kuwa meusi!
1. Unyoaji…. Wembe unachangia sana kuwa na makwapa meusi…ile
puruuu puruuuu aaah mwenzangu lazima kwapa lidate hahahahaaa…. Hapo umetia
vijisabuni kidogo unashave kwa nguuuuvu ili kwapa libaki jeupe mpaka mtu nje anaweza uliza jamani kuna usalama uko? anhaaaa!!
2. Deodorant:… unaroll deodorant wiki ya kwanza…ya pili..ya tatu…unaona
mabadiliko kwapani we umo tu!.... kipodozi chochote kikionyesha hali ya
kukukataa hata kama ni siku mbili tatu…KIACHE!! Ukijitia una uchungu na hela
yako utagharamamika zaidi ya hizo ulizotoa kwenye kutibu matokeo, unapaka
deodorant unasikia kwapa linawaka moto
jamani bado umo tu! yahusu!
3. Magonjwa… hapa sitaingia sana maana sina utaalamu huo ila
ndio hivyo kuna wakati hali hiyo inaletwa na ugonjwa ulionao na utagundua hili
kama njia zingine zote zikidunda.
Haya sasa ndio tushapata kwapa jeusi...tufanyeje?
NAMNA YA KUKABILIANA NA KWAPA JEUSI
1. LIMAO NA SUKARI
Hii njia ya kwanza iliyo bora kabisa na nyepesiiii
Kata kipande cha limao kichovye kwenye sukari, tena ile ya
brown ndio nzuri zaidi.
Sugua kwapa lako kwa mtindo wa kuzunguka. Taratibu tu ila
hakikisha unasugua eneo zima. Usikamue limao wewe sugua tu…majimaji yatatoka yenyewe.
Acha kwa dakika 10-15 kisha osha makwapa yako vizuri kwa
sabuni yako ya kila siku.
Fanya hivi asubuhi na jioni mpaka uone weusi umeondoka na lazima uondoke.
Faida yake ni kuwa Limao litaondoa pia harufu ya kwapa, na
katika kipindi hiki usipake deodorant yoyote.