Lee Min Ho
Nilikosa tu kazi ya kufanya
nikajikuta natamani kuangalia chochote cha kunichangamsha…. Katika harakati za
kutafuta kiburudisho nikaletewa CD ya series ya kikorea…. Mimi ni mpenzi mkubwa
wa series za kikorea .… kuanzia zile za kihistoria mpaka za kisasa, weka
mapenzi na maisha au visasi na vita kwa wakorea hunibandui kwenye kiti!
Safari hii nikakumbana na hii
series ya CITY HUNTER!... Wakati naanza kuiangalia kidogo nighairi na kuiweka
kando lakini saa moja mbele nikajikuta nang’ang’ania kuiangalia masaa. Sio tu
kwa utamu wa hadithi na maudhui yake bali pia kwa waigizaji mahiri walioshiriki
hususani muigizaji mkuu LEE MIN HO!!
Aisee!... ni miaka mingi sijakaa
kwenye Tv nikatazama kitu kwa usongo na kuvutiwa na muigizaji wa kiume kiasi
cha kuhisi nawehuka…ila kwa Lee Min Ho heheheeee I had to rewind and rewind
some parts of the series and guess
what….i couldn’t get it enough LOLEST!!
Mkorea Lee Min Ho
Ni ndani ya miezi miwili tangu
niitazame Ciy Hunter…. Na tayari nimeshatazama series zake zingine tatu…
kuna hiyo City Hunter …. Hii ni ya kipelelezi, visasi na karate za
kutosha, mtoto anaibiwa toka kwa mama yake, aliyemuiba ni rafiki wa marehemu
baba wa mtoto. Anamkuza porini uko kama mwanaye kisha amatuma mjini kulipa
kisasi… yanayoendelea hapo hadi mtoto kuja kugundua kisasi anacholipisha ni kwa
maslahi ya baba mlezi tu… ngoma imeranduka vibaya mno! Piga nikupige
zimeshatembea vya kutosha!
Kuna hii Personal
taste…. Hii bwana Jamaa mtu wa michoro ya ramani, baada ya mzee wake
kudhulumiwa mali akaamua kufungua kampuni yake akihangaikia tenda hapa na pale
ili afikie malengo… katika kutafuta namna ya kushinda tenda ambayo
anaishindania na kijana mwenzake ambaye baba yake ndiye aliyewadhulumu akina
Lee min ho…
SOMA ZAIDI....