4
Sehemu ya nne
Njia nzima Sindi na Jerry walibishana hiki na kile,
wakaelezana haya na yale. Kwa muda mfupi tu waliozungumza njiani Jerry
aligundua Sindi Nalela alikuwa na upeo mkubwa tofauti na elimu yake ya shule ya
msingi aliyokuwa nayo.
Pasipo kujua Nyanza alikuwa akiwafuatilia nyuma, walisimama
na kubishana, wakisontana kwa vidole na mara kadhaa Jerry akikwepa vibao vya
Sindi pale alipomtania na kumcheka. Nyanza aliyaona yote haya na aliyafuatilia
kwa umakini mkubwa mpaka pale alipohisi asingeweza kuwafuatilia tena baada ya
Sindi na Jerry kuagana na kila mmoja kushika njia yake.